Chagua Skills Sahihi
Pata mafunzo ya vitendo katika Graphic Design, Video Editing, Social Media Management na Digital Marketing.
Soko la ajira linahitaji vijana wabunifu pamoja na wataalamu wenye ujuzi unaoweza kutatua changamoto katika makampuni au biashara.
Kupitia mafunzo yetu ya vitendo, tunakupa maarifa sahihi na ya wakati sahihi yatakayokutengenezea fursa za kiuchumi kupitia ulimwengu wa kidijitali.
Pata mafunzo ya vitendo katika Graphic Design, Video Editing, Social Media Management na Digital Marketing.
Maliza kozi zako na upate cheti kinachotambulika, kikuzae nafasi za ajira na ushindani sokoni.
Tunatoa usimamizi kutoka Beginner hadi Expert, tunakupa uzoefu wa majukumu halisi ya kazi.
Jukwaa hili limeanzishwa rasmi ikiwa na shauku kubwa ya kuboresha mfumo wa elimu ya vitendo kwa vijana nchini Tanzania. Dhamira yetu kuu ni kuziba pengo lililopo kati ya elimu ya darasani na soko halisi la ajira.
Tunatoa usimamizi kwa wanafunzi wanaotaka kubobea katika Graphic Design, Video Editing, Social Media Management, na Digital Marketing katika level kubwa ya ushindani wa soko la Tanzania.
Soma zaidi
Chagua kozi inayokufaa na uanze safari yako ya kujifunza
Hakuna kozi au vitabu vilivyopatikana kwa sasa.
Siku zote katika kujifunza ujuzi wa kidijitali hakikisha unachagua kozi sahihi, njia sahihi ili kupata matokeo bora kwa muda sahihi.
Browse All CoursesHakuna kozi kwa sasa.
Namna ambavyo jukwaa letu limeweza kubadilisha mtazamo wa vijana katika kujenga uchumi katika soko la mtandao na kuhakikisha wanatengeneza ajira binafsi na hata kuajiriwa.
Wanafunzi
Jumuiya
Kozi Zilizopo
Vyeti Vilivyotolewa
Skills zinazohitajika sana kwenye soko la ajira Tanzania
Huu ndio utaratibu rahisi wa kupata mafunzo Brandkidigitali Academy.

Mwanafunzi anaanza kwa kujenga msingi thabiti kupitia Recorded Videos zilizokamilika pamoja na vitabu vya muongozo kwa lugha ya kiswahili. Hatua hii inampa uhuru wa kujisomea mahali popote na muda wowote unaomfaa kabla ya kuingia darasani.

Mafunzo haya yanatumia mbinu kamili (Action-Based Learning Approach), ambapo kila hatua ya masomo inaambatana na mazoezi ya vitendo (assignments). Mbinu hii haikupi tu nadharia, bali inakutaka utumie ujuzi papo kwa papo ili kujenga uzoefu wa kazi halisi za sokoni, ukijengewa uwezo na utayari kuajiriwa.

Wanafunzi wote wanaojiunga na mafunzo wanaunganishwa na Group la Whatsap. Mfumo huu unakuunganisha moja kwa moja na wakufunzi waliobobea kwa ajili ya kupata msaada wa haraka wa changamoto zako, huku ukishirikiana na wanafunzi wenzako jambo linaloongeza hamasa, kasi ya kujifunza, na mtandao (networking) wa kitaalamu.

Mafunzo haya yanatumia mbinu ya "Kujenga Matokeo Yanayoonekana" (Outcome-Based Learning Approach), ambapo baada ya kukamilisha masomo na miradi yote ya vitendo, utapatiwa cheti rasmi cha kuhitimisha pamoja na portfolio thabiti ya kazi zako. Mfumo huu haukupi tu cheti, bali unakupa ushahidi kamili unaokuwezesha kujiamini wakati wa kuomba kazi.